Maandamano makubwa DDR ya Novemba 4, 1989
4 Novemba 2019Maelfu kadhaa ya wapinzani walidai wakati huo pamoja na wawakilishi wa serikali kuwapo na mageuzi ya kisiasa. Hata hivyo kitengo cha usalama wa taifa maarufu kama Stasi kilikuwa kimeingiwa na hofu.
Kulikuwa tayari na tetesi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani , DDR. Wananchi kwa miezi kadhaa walikuwa wanapima kujitoa kutoka katika maficho na kuingia mitaani. Mjini Leipzig walikuwa watu wakiandamana kila mwezi kwa ajili ya uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kusafiri wapendako. Zaidi na zaidi wananchi wa nchi hiyo wamekuwa wakiipa kisogo nchi hiyo inayofilisika kisiasa pamoja na kiuchumi. Utawala wa kikomunisti wa DDR ulikuwa ukiwaita watu wenye mwelekeo huo kuwa ni wakimbizi wanaoikimbia jamhuri hiyo.
Erich Honecker , ambaye kuanzia mwaka 1973 alishika madaraka ya nchi hiyo, aliondolewa madarakani Oktoba 18. Lakini hata mrithi wake Egon Krenz hakupata uungwaji mkono na wananchi wake. Kutokana na hali hii tarehe 4 Novemba 1989 yalifanyika rasmi maandamano makubwa yaliyopata kibali katika historia ya Ujerumani mashariki DDR.
Waliotayarisha ni wacheza sinema na watu wanaohusika katika maigizo ya tamthilia kutoka Berlin mashariki. Walidai kuhusu vifungu vya katiba 27 na 28 , ambavyo ni uhuru wa kutoa maoni,uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kukusanyika. Vifungu hivi kwa muda wa miaka 40 ya DDR vilikuwapo tu kwa nadharia.
Katika siku hii lakini katiba ambayo kwa muda mrefu ilikanyagwa ilirejeshewa uhai na kundi kubwa la binadamu waliojitokeza katika uwanja wa Alexanderplatz mjini Berlin.
Makadirio yanatofautiana miaka 30 baadae kwamba watu 200,000 na milioni moja walishiriki katika maandamano hayo.
Kiongozi wa chama tawala
Kile walichokishuhudia kilikuwa ni hali ya kipekee kabisa katika historia ya Ujerumani mashariki. Waandamanaji walikusanyika mbele ya gari ndogo ya kubeba mizigo, na katika eneo dogo la uwazi kati ya maduka kuliwekwa jukwaa dogo la mbao. Hilo lilikuwa jukwaa lililotumiwa na zaidi ya wazungumzaji 20. Wacheza sinema, waimbaji, watunzi wa vitabu, na wachungaji na mapadre, lakini pia wawakilishi wa utawala.
Mmoja miongoni mwao alitokea kuwa maarufu siku tano baadaye, Novemba 9 , 1989 duniani kote. Guenter Schabowski, mwenyekiti wa chama tawala mjini Berlin cha Sozialistishe Einheitspartei Deutschland, SED.
Katika hali hii alitangaza katika mkutano na waandishi habari sheria mpya iliyohusu watu kusafiri, hatua ambayo ilisababisha kwa hali ya mshangao kuja kuanguka kwa ukuta wa Berlin. Katika maandamano ya tarehe 4, Novemba Schabowski alizomewa sana na waandamanaji.
Hata pale alipoanza kusema , "tunaidhinisha utamaduni wa kujadiliana".
Watendaji wa utawala wa kikatili wa DDR katika wakati huu walikuwa wamepoteza kila aina ya uaminifu. Hatua ya Schabowski ya kujikosoa ilizimwa na kelele za waandamanaji.
Ukomunisti waanguka
"Ni nini kinaweza kuuendesha ukoministi katika mtazamo huu na mwelekeo huu wa maelfu ya watu ?" Aliuliza kundi hilo kubwa la watu ambao bila shaka walikuwa wana mtazamo wa chuki dhidi yake. Jibu lake binafsi lilikuwa , "Ni yule tu anayesikia na kuelewa onyo, anaweza kuanza upya."
Mmoja wa watu ambao waliyachukua maneno ya Schabowski , alikuwa mkosioaji mkubwa wa utawala wa DDR Friedlich Schorlemmer. Mwanathiolojia huyo kutoka Wiitenberg, mji alikozaliwa muasisi wa mageuzi katika kanisa la kiluteri , Martin Luther, alinukuu mabadiliko ya wimbo wa taifa wa DDR: "Majira ya Mapukutiko mwaka 1989 tulikubaliana kubadilisha magofu na kujenga upya mustakabali wetu." Kutokana na hisia za wakimbizi wengi wa DDR aliwataka wananchi kubakia katika eneo hilo, na kuijenga upya nchi hiyo. Hivi sasa tunamhitaji kila mmoja wetu."
Mcheza sinema kijana Jan-Josef Liefers, ambae katika Ujerumani ya sasa iliyoungana amekuwa maarufu katika kipindi cha televisheni cha Tartort, aliwatupia swali la wazi viongozi wa chama cha SED: Kwa kuwa viongozi wa juu wa SED wanachukua hatua kutokana na mbinyo kutoka kwetu, mtazamo wangu ni kwamba jukumu lao la hapo zamani halistahili tena kuzungumzwa.
Kundi kubwa la watu katika uwanja wa Alexanderpatz lilitaka kusikia maneno kama hayo.
Kulikuwa na shangwe kubwa.