Maandamano mapya kuhusu muswada wa pensheni Ufaransa
15 Machi 2023Hatua ya karibuni zaidi katika mchakato huo wa kutunga sheria ya kuongeza umri wa kistaafu kutoka miaka 62 hadi 64inazusha kilele cha mvutano wa kisiasa wakati swali likiwa ni kama utapata uungwaji mkono kwa wingi bungeni.
Mkutano huo wa maseneta saba na wabunge saba unalenga kupata muafaka wa rasimu ya mwisho.
Soma pia:Bunge la Seneti Ufaransa laidhinisha mageuzi ya mfumo wa pensheni
Baraza la Seneti linatarajiwa kuuidhinisha mswada huo kesho kwa sababu wajumbe wa Kihafidhina walio wengi wanaunga mkono kurefushwa umri wa kustaafu.
Hali hata hivyo ni tofauti katika bunge la kitaifa ambako Macron hana wingi wa viti.
Wakati huo huo, vyama vya wafanyakazi vinatumai kuwa maandamano yao kote nchini yataendelea kuonyesha upinzani mkubwa wa wafanyakazi kwa mpango huo, unaopigiwa debe na Macron anayeuona kama utakaoufanya uchumi wa Ufaransa kuwa na ushindani mkubwa.