1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Maandamano mapya ya WaSerbia yaibuka Kosovo

31 Mei 2023

Maandamano mapya ya watu ya jamii ya Waserbia walio wachache huko Kosovo yamezuka tena leo kaskazini mwa nchi hiyo.

Waandamanaji wa jamii ya Serbia wakiwa wameshika bendera kubwa ya taifa lao wakati walipoandamana mbela ya ofisi ya jiji, katika manispaa huko, Zvecan Mei 31, 2023.
Maandaano ya jamii ya walio wachache ya Serbia waishio Kosovo wamekuwa wakifanya maandamano ya kumpinga meya mpya wa eneo hilo mwenye asili ya Albania.Picha: Bojan Slavkovic/AP/picture alliance

Hata hivyo, tovuti ya habari ya koha.net umeripoti kuwa hali imeendelea kuwa tulivu. Ghasia kati ya wanamgambo wa Serbia na ujumbe wa kulinda amani wa Jumuia ya Kujihami ya NATO, KFOR huko Zvecan yalisababisha majeraha kwa wanajeshi 30 na Warsebia 50. Awali, NATO ilitangaza kupeleka wanajeshi zaidi 700 ili kukisaidia kikosi cha wanajeshi 3,800 kilichoko Kosovo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken ametoa wito wa kuwepo utulivu. Akizungumza na kituo cha utangazaji cha Marekani, CNN, Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti amesema anahitaji kuwa na askari polisi wanaotetea utawala wa sheria, wanaolinda utulivu, amani na usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW