Nchini Msumbiji watu sita wanaaminika kuwa wameuawa baada ya ghasia kuzuka wakati wa maandamano ya kupinga ogezeko la bei za bidhaa muhimu za matumizi, kama vile unga, mkate na mafuta
Matangazo
Inasemekana watoto wawili walipigwa risasi, na watu wengine wanne wameuawa baada ya machafuko hayo. Duru zinaeleza kuwa polisi walifyatua risasi hewani ili kuutawanya umati wa watu waliokuwa wanaandamana katika mji mkuu, Maputo.