1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano nchini Brazil

Admin.WagnerD5 Septemba 2016

Maelfu ya raia wa Brazil walifanya maandamano ya kumuunga mkono rais aliyefutwa kazi Dilma Rousseff na kukashifu serikali mpya ya Michel Temer aliyechukuwa mamlaka na kupuuza maandamano hayo.

Polisi katika mji mkubwa nchini brazil Sao Paulo walikabiliana na waandamanaji waliofanya maandamano ya kumkataa rais mpya Michel Temer siku tano baada ya Dilma Rousseff kung'atuliwa kama kiongozi wa nchi hiyo kubwa zaidi katika eneo la Amerika Kusini.

Kizuizi cha moto kilichowekwa na waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga kesi dhidi ya Dilma Rousseff.Picha: picture-alliance/dpa/R.Rosa

Waandalizi wa maandamano hayo waliokataa uteuzi wa Temer na kuutaja kama mapinduzi ya serikali walisema kuwa maelfu ya waandamanaji walimiminika katika barabara za Paulista wakibeba mabango yaliyokuwa yameandikwa, Temer aondolewe na uchaguzi ufanywe sasa.

Maafisa wa polisi mjini Sao Paulo walisema kuwa iliwabidi kutumia vitoa machozi kuzuia wizi na uharibu uliokuwa ukitekelezwa katika maandamano hayo dhidi ya rais Michel Temer.

Katika taarifa, idara ya usalama wa umma ilisema kuwa kundi moja lilianzisha ghasia katika barabara moja ya nchi hiyo na pia kuwarushia mawe polisi baada ya maandamano hayo.

Mapema hii leo watu walikuwa wamekusanyika katika eneo la matembezi la Copacabana jijini Rio de Janeiro kutaka Temer kuondolewa mamlakani na uchaguzi mpya kuandaliwa.

Temer apuuza maandamano

Temer ambaye baada ya kuapishwa kuwa rais alisafiri nchini China kuhudhuria mkutano wa G20 alisema kuwa maandamano hayo yalifanywa na makundi madogo ya watu,,,,aliongeza kwa kusema "sina idadi kamili ya walioandaa maandamano hayo lakini nadhani ni watu kati takriban 40, 50 ama 100. hao si watu wengi ikilinganishwa na raia milioni 204 wa Brazil kwa hivyo hatua hiyo haina maana yoyote".

Wafuasi wa rais aliyeng'atuliwa mamlakani Dilma Rousseff mjini Sao Paulo wakifanya maandamano .Picha: picture-alliance/dpa/S. Moreira

Hata hivyo upande wa upinzani ulipuuza kauli hiyo ya rais na kulingana na mwanachama mmoja wa makundi hayo ya upinzani yaliyoandaa maandamano hayo Guilherme Boulos, tayari watu elfu 100 wamekusanyika katika barabara ya Paulista kukosoa uteuzi huo wa Tremer.

Kulingana na aliyekuwa seneta na mgombea wa sasa wa baraza la mji wa Sao Paulo Eduardo Suplicy Maandamano hayo yana maana yake,.....insert OTON

Rousseff atangaza upinzani

Rais aliyetimuliwa Dilma Rousseff hata hivyo ameapa kumpa upinzani mkubwa Temer aliyekuwa makamu wake. Amewasilisha rufaa katika mahakama ya juu ya nchi hiyo dhidi ya hatua ya kuondolewa kwake afisini lakini wataalamu wa maswala ya kisheria wanasema kuwa huenda rufaa hiyo isifanikiwe kwa sababu rufaa nyingi zilizowasilishwa wakati wa hatua ya kumng'atua mamlakani iliyochukuwa zaidi ya mwezi mmoja zilikataliwa.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha habari cha kigeni siku ya Ijumaa, Rousseff alisema kuwa atapaza sauti yake iwapo serikali ya Temer itajaribu kuwanyanyasa waandamanaji. Siku chache kabla na baada ya kuondolewa kwake, baadhi ya maandamano dhidi ya Temer yalitawanywa na polisi.

Katika kikao cha wanahabari wakati wa mkutano wa G20 nchini China kabla ya maandamano ya Sao Paulo, Temer alisema kuwa waandamanaji watakaoharibu mali watachukuliwa hatua na kwamba hayo hayatakuwa maandamano bali uhalifu.

Uchaguzi mpya utaandaliwa tu iwapo Temer atajiuzulu kabla ya mwisho wa mwaka , Kung'atuliwa mamlakani ama kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo kuwa hafai kushikilia wadhifa huo kwa madai ya kasoro za kampeini wakati wa uchaguzi wa mwaka 2014.

Mwandishi: Tatu Karema/afp/ap

Mhariri: Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW