Maandamano nchini Ukraine
5 Aprili 2007Matangazo
Waziri mkuu Viktor Yanukovych katu katu amekataa kuitambua amri hiyo iliotolewa jana, na amesema ataungojea uamuzi wa mahakama kuu ya kikatiba.
Saumu Mwasimba alizungumza na mwandishi wetu katika mji mkuu wa Ukraine,Kiew, Mohammed Masoud, na akamuuliza vipi ilivyo sasa vuta ni kuvute hii baina ya wanasiasa hao wawili ilioanza hata kabla ya mapinduzi ya machungwa ya mwaka 2004 yaliomweka madarakani Rais Yushenko.