MAANDAMANO YA JUMATATU HUKO MASHARIKI MWA UJERUMANI JUU YA SOKO LA KAZI,FIDIA YA LIBYA KWA WAHANGA WA BOMU KATIKA DISCO YA LA BELL HUKO BERLIN NI MIONGONI MWA MADA ZA WAHARIRI LEO:
12 Agosti 2004GAZETINI:
Kuhusu mjadala wa soko la kazi gazeti la Frankfurter Rundschau laandika juu ya
" Maandamano ya jumatatu ya kupinga mapedekezo ya kile kinachoitwa HARTZ IV, Ghadhabu zilizoiubuka chamani pamoja na hasira miongoni mwa vikundi vya wabunge wa serikali ya muungano.Kanzela Gerhard Schröder na Mwenyekiti wa chama-tawala cha SPD Franz Münterfering wanapaswa sasa kuchukua hatua na wakiungana na chama cha KIJANI lazima watie breki.
Hiyo ni breki itakayokua na athari zake.Kwani ndani ya baraza la mawaziri patazuka dharuba kali."
Waziri wa fedha Hans Eichel na waziri wa uchumi Wolfgang Clement hujikuta hawana la kusema au kielezo tangu wanapoondoa uwezekano wa kuzuka upungufu katika sehemu ya pili ya malipo ya wasio na kazi hapo januari mwakani na hata katika kutoa uhakikisho kuwa muda wa masomo ya kazi katika kuweka vipimo wazi vya malipo kwa wasio na kazi hautahesabiwa.Kwa muda mrefu waziri wa fedha daima akiadi hakuna fedha zaidi.Na pia daima hakuna njia nyengine."
Hilo lilikua FRANKFURTER RUNDSCHAU.
Ama gazeti la DIE WELT laandika:baada ya kurudi likizo,amewafanya mawaziri wake wa fedha na uchumi kufanya hesabu ya gharama ya likizo yake .Amekutana nao kuzungumza jinsi serikali itavyoweza kuzima jaziba ili0panda humu nchini.
Jukumu la jaziba hiyo linatupwa na wengi mabegani mwa Idara ya habari ya serikali ya shirikisho-BUNDESPRESSEAMT.
Kimsingi, kuanzisha kampeni ya kueneza habari baada ya balaa la malalamiko ya jumatatu huko Mashariki mwa Ujerumani tayari limezushwa na waandamanaji , bila shaka si kazi njema kwa idara hiyo."
Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG likitugeuzia mada na kutuchukua katika kesi ya ugaidi ya Mmorocco Motassadeq ,laandika kwamba,
mnamo miezi michache iliopita, waziri wa ndani Otto Schily ,waziri wa sheria Brigitte Zypries na mshtaki mkuu wa serikali Kay Nehm walijitahidi kweli kuwashawishi Wamarekani kwamba Bin al-Schibb anahitajika kuwapo kizimbani katika kesi hii hapa Ujerumani.Kisheria hii inaingia akilin, lakini kuitarajia Marekani kuitikia dai hilo ni upumbavu.Kwani mtu kama al-Schibb akiwa mikononi mwa shirika la ujasusi la Marekani CIA, hawamtoi asilani kwa ulimwengu wa nje. Hawamtoi hata kwa Mahkama ya Marekani au Halmashauri ya Baraza la Senate la Marekani.Hizo ndizo sheria za Idara za usalama na ujasusi."-laandika gazeti.
Nalo gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND kutoka Hamburg lasangaa hasa kuhusu serikali ya Marekani:
laandika:
Kwanza Marekani kwa ujeuri iliiarifu Mahkama ya Ujerumani huko Hamburg kwamba hata katika mashtaka haya ya pili aliofunguliwa Mounir al-Motassadeq, hawatamleta shahidi muhimu kwa kesi hii.Halafu sasa wametuma Fax ambayo sio njia ya siri kabisa kutumiana habari za siri kuwa watayari kutuma dafutari ambalo lingemsaidia hakimu kuhukumu.Ili mtuhimiwa huyu wa hujuma ya ugaidi apewe hukumu anayostahiki,Mahkama ya hamburg lazima ipate dafuitari hilo.lakini Marekani inakataa kabisa kufanya hiovyo.Kwahivyo, wamarekani wasistaajabu ikiwa mwishoe hukumu itapitishwa ambayo hawataipenda-lamaliza FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND.
Tukibadili tena mada tunaelekea sasa masikizano yaliofikiwa ya kulipa fidia Libya kwa wahanga wa hujuma ya Bomu katika Disco ya ‘LA BELLE’:Kufuatia masikizano hayo, Kanzela Schröder sasa anapanga kuzuru Libya.
Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE laandika:
"Ziara aliotangaza Kanzela Schröder kuifanya Libya katika robo ya mwisho ya mwaka huu imekuja wakati muafaka ili kuarifu uongozi wa Libya kwamba daraja iliowekwa na kambi ya magharibi kuwa na usuhuba wa aina mpya na Mashariki ya kati, haittatosha tu kujenga mahusiano bora ya kiuchumi. Katika siasa mpya na nchi zinazopakana na bahari ya Kati ,Umoja wa Ulaya unaambatisha sharti kuwa lazima Gaddafi ahishimu kwa jumla haki za binadamu na hapa anasubiriwa kuhetimu mtihani mmoja hadi mwengine."