1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kupinga chama cha AfD kufanyika Ujerumani

Saleh Mwanamilongo
12 Januari 2025

Maandamano ya muungano wa wanaharakati wa Ujerumani yameanza kufanyika Jumamosi kukipinga cha chama cha mrengo mkali wa kulia cha Ujerumani cha AfD.

Maandamano ya kupinga chama cha AfD kufanyanika Saxony mashariki mwa Ujerumani
Maandamano ya kupinga chama cha AfD kufanyanika Saxony mashariki mwa UjerumaniPicha: EHL Media/IMAGO

Waandalizi wanatarajia zaidi ya watu 10,000 kuhudhuria maandamano dhidi ya AfD. Waandamanaji kutoka takriban miji 70 wanatarajiwa kuwasili katika mabasi zaidi ya 100 yaliyokodishwa kwa tukio hilo.

Hatua hiyo inafuatia kufunguliwa leo kwa mkutano wa siku mbili wa chama cha AfD huko mjini Riesa, jimbo la Saxony, mashariki mwa Ujerumani.

Waandamanaji pia walipanga kuzuia njia za ufikiaji kwenye ukumbi ambapo mkutano wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD utafanyika.

Mamlaka za jimbo la Saxony zimepeleka polisi wa kuzuiya ghasia. Uchaguzi wa bunge nchini Ujerumani unapangwa kufanyika Februari 23.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW