1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kupinga marufuku ya Hijab katika shule za Ufaransa:

18 Januari 2004
PARIS: Nchini Ufaransa na nchi kadha nyingine, Waislamu elfu kadha wamefanya maandamano makubwa ya kupinga uamuzi wa kupigwa marufuku vazi la Hijab katika shule za Kifaransa. Peke yake mjini Paris waliandamana Waislamu 5000. Maandamano mengine makubwa yalifanyika katika miji ya Marseille na Mülhausen. Pia katika miji ya London, Brussels, Bahrein, Beirut, Amman, Ghaza na Ankara yalkifanyika maandamano makubwa mbele ya Balozi za Ufaransa. Pamoja na Hijab, msswada huo wa sheria ulioshauriwa na Rais Jacques Chirac, una shabaha ya kupiga marufukui uvaaji wa vikofia vya Kiyahudi na misalaba katika shule za Kifaransa.