1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kupinga serikali Iran yamemalizika

Sekione Kitojo
3 Januari 2018

Uturuki imesema hatua alizochukua Rais Hassan Rouhani wa Iran kushughulikia siku kadhaa za maandamano zilikuwa sahihi na Uturuki inathamini uthabiti wa Iran.

Iran Demonstration für die Regierung
Picha: Reuters/Tasnim News Agency

Matamshi hayo ni ya kwanza ya uungaji mkono kutoka kwa viongozi wa kanda hiyo. Wakati  huo  huo ujerumani  imesema .inafuatia yale yanayotokea  nchini  Iran  ikiwa  na  wasi  wasi , lakini imesisitiza  kwamba  waandamanaji  wanaoandamana kupinga  ughali  wa  maisha  wanapaswa  kuheshimiwa.

Chanzo  katika  ofisi  ya  rais  wa  Uturuki Recep Tayyip Erdogan  kimesema  rais  alijadili  machafuko  ya  wiki nzima  nchini  Iran  wakati  akizungumza  na  rais Rouhani kwa  simu. Rais  wa  Iran  alimwambia  Erdogan  ana matumaini  maandamano  yatamalizika katika  siku chache ",  chanzo  hicho kimesema.

Mamia  ya  Wairan walishiriki  katika  maandamano  ya kuiunga  mkono  serikali  katika  miji  kadhaa  leo  katika kile  kinachoelezwa  kuwa  ni  tukio  lililotayarishwa  na serikali  kuonesha  nguvu  zake  baada  ya  siku  sita  za machafuko   mitaani  ambayo  yameutikisa  uongozi  wa kidini  na  kusababisha  watu 21  kuuwawa.

Haki ya kuandamana

Rouhani  alisema  siku  ya  Jumapili  kwamba  Wairani wana  haki  ya  kuandamana  na  kutumia  mamlaka  yao lakini  hatua  zao  hazipaswi kusababisha  ghasia, fujo  na kuharibu  mali  za  watu. Muandamanaji  mjini Tehran Mohammad Hossein Vakili  amesema  waandamanaji  wako makundi  mawili.

Maandamano ya kuiunga mkono serikaliPicha: Fars

"Waandamanaji  wamegawanyika  katika  makundi  mawili. kundi  moja linaandamana kwa  kweli  na  lingine  linafanya ghasia. kitu cha  kwanza  serikali  inapaswa  kuweka mipaka  kati  ya  waandamanaji  na  wafanyaghasia. Ni jukumu  zito  na  sijui, lakini  viongozi  wa  juu  wa  serikali wanapaswa  kutafuta  suluhisho. Wasitoe  adhabu  kwa wahalifu  na  watu  wasio  na  hatia  bila  kutenganisha. Kwanini  wanikamate  mtu  kama  mimi wakati naandamana kwa  kupinga  kupanda  bei  ya  mayai?"

Erdogan  amemwambia  Rouhani , kwamba  anayaona matamshi  yake  juu  ya  waandamanaji  kutokiuka  sheria wakati  wakitekeleza  haki  yao  ya  kuandamana  kwa amani kuwa  ni  sahihi," chanzo  hicho kimesema.

Waandamanaji wakibeba mabango yanayoilaani Israel na MarekaniPicha: Reuters/Tasnim News Agency

Msemaji wa  serikali  ya  Ujerumani  Ulrike Demmer amesema  serikali  yake  inaona  kuwa  ni  haki wakati  watu wakiandamana  mitaani  kupinga  matatizo  yao  ya kiuchumi  na  kisiasa  kama  ilivyotokea  nchini  Iran  kama ilivyo  tokea  na  tunawaheshimu.

Wakati  huo huo rais Donald Trump amesema  kwamba ataonesha  uungaji  wake mkono kwa  waandamanaji nchini  Iran  katika  wakati  muafaka, ikiwa  ni  matamshi yake  ya  hivi  karibuni  kabisa  kupitia  ukurasa  wa  Twitter.

Lakini  kamanda wa  jeshi  la  mapinduzi  nchini  Iran Mohammed Ali  amesema  maandamano  ya  wanaoipinga serikali nchini  humo  yamemalizika.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW