1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi kufanyika Ufaransa

23 Septemba 2023

Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi yamepangwa kufanyika kote nchini Ufaransa leo hii, ikiwa ni takriban miezi mitatu baada ya kifo cha mvulana mwenyse asili ya Kiarabu

Frankreich I Ausschreitungen und Proteste halten an
Picha: Clement Mahoudeau/AFP

Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi  yamepangwa kufanyika kote nchini Ufaransa leo hii, ikiwa ni takriban miezi mitatu baada ya kifo cha mvulana mwenyse asili ya Kiarabu wakati wa ukaguzi wa polisi katika kituo kimoja karibu na mji mkuu, Paris. Waandaaji wametoa wito wa mikusanyiko katika jiji la Paris na miji mingine. Waandamanaji wanagadhibishwa na ubaguzi wa kimfumo, ongezeko la kutokuwa na usawa katika jamii, hali ambayo kimsingi inaathiri wakaazi wa vitongoji masikini, wengi wao wakiwa Wafaransa wenye asili ya Kiarabu na Kiafrika.Nahel, kijana aliyekuwa na umri wa miaka 17, aliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi katika mkasa ambao ulizusha ghasia zilizoambatana na matukio ya uchomaji moto na uporaji, zilizodumu kwa siku kadhaa na kuathiri taifa zima.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW