Maandamano ya kupinga vita vya Iraq katika mkutano mkuu wa Republican
2 Septemba 2008ST PAUL MAREKANI
Polisi wakukabiliana na fujo wamapambana na waaandamanaji waliona hasira wanaopinga vita nchini Iraq kabla ya kuanza mkutano mkuu wa chama cha Republican.
Polisi waliwatawanya waandamanaji hao wakitumia gesi ya pili pili na mabomu ya moshi ambapo pia waliwakamata kiasi cha waandamanaji 130.
Watu hao waliandamana kutoka mji mkuu wa jimbo la Minessota hadi mahala ambako mgombea wa urais wa chama cha Republican John McCain anatazamiwa kukubali rasmi uteuzi huo baadae wiki hii.
Aidha inaripotiwa kwamba waandamanaji hao wanataka vita vya Iraq vimalizwe,na pia haki za wahamiaji nchini Marekani ziongezwe halikadhalika Marekani ibadili sera zake nchini Ethiopia.
Wengi wa waandamanaji hao kiasi cha 10,000 walikuwa wamevalia fulana za kumuunga mkono mgombea wa urais wa chama cha Demokratic Barack Obama.Wakati huohuo inaarifiwa kimbunga cha Gustav kimepungua makali.