1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya Ubelgiji yageuka kuwa vurugu

24 Januari 2022

Takriban watu 50,000 walijitokeza mitaani kuandamana  huko  Brussels jana kupinga hatua za  kiafya zinazochukuliwa na mamlaka ya Ubelgiji.

Belgien | Coronavirus | Proteste und Ausschreitungen in Brüssel
Picha: Hatim Kaghat/BELGA MAG/AFP/Getty Images

Baadhi ya maandamano yaligeuka kuwa vurugu ambapo kiasi watu 70 walikamatwa wakati wa maandamano hayo. Watu hao walikamatwa baada ya kukutwa na vifaa hatari au vilivyopigwa marufuku na wengine walikamatwa kwa kufanya uharibifu wa mali kwa mujibu wa msemaji wa polisi.

Maafisa watatu wa polisi na waandamanaji 12 walipelekwa hospitali baada ya kujeruhiwa.

soma zaidi: Ulaya yaimarisha vizuizi vya kukabiliana na virusi vya corona

Waziri mkuu wa Ubelgiji De Croo aliyalaani kwa maneno makali maandamano hayo akisema kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake lakini jamii  haiwezi kuruhusu vurugu. Waandamanaji walionekana wakipeperusha bendera za Ujerumani, Poland na Ufaransa miongoni mwa nyingine.

Aidha walibeba mabango yaliyokuwa na maandishi ya kupinga chanjo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW