1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMadagascar

Maandamano ya vijana wa GenZ yaendelea kushuhudiwa Afrika

5 Oktoba 2025

Maandamano ya vijana maarufu kama GenZ yameendelea kuyatikisa mataifa kadhaa ya Afrika ambapo waandamanaji wanadai uwajibikaji wa viongozi na uwepo wa huduma bora za kijamii.

Antananarivo 2025 | Vijana wakiandamana katika mji mkuu wa Madagascar
Vijana wakiandamana katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo wakimtaka rais kujiuzuluPicha: Zo Andrianjafy/REUTERS

Huko nchini Madagascar waandamanaji walimiminika jana katika mitaa ya mji mkuu Antananarivo wakimtaka rais  Andry Rajoelina  kujiuzulu, harakati ambazo rais huyo amezitaja kuwa jaribio la mapinduzi. Umoja wa Mataifa umesema hadi sasa watu 22 wameuawa huku mamia ya wengine wakijeruhiwa.

Nchini Morocco, vijana waliandamana kwa siku ya nane mfululizo hapo jana wakidai uwepo wa huduma bora za afya na elimu. Hivi majuzi maandamano hayo yaligeuka kuwa ya vurugu na kusababisha vifo vya watu wawili huko Agadir, kitendo kilichozidisha hasira ya waandamanaji katika  taifa hilo la Kifalme.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW