1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Maandamano yaendelea Georgia kwa siku ya saba mfululizo

5 Desemba 2024

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Georgia, Tbilisi, dhidi ya serikali ya kitaifa ya kihafidhina, ikiwa ni kwa usiku wa saba mfululizo.

Georgia | Tbilisi | Maandamano
Polisi wamefunga barabara ili kuzuia waandamanaji wanaoandamana kupinga uamuzi wa serikali kusitisha mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.Picha: Zurab Tsertsvadze/AP Photo/picture alliance

Waandamanaji hao walifunga barabara kuu ya Rustaveli na kutoa wito wa muendelezo wa sera zinazouunga mkono Umoja wa Ulaya kwa taifa hilo, kufuatia uamuzi wa chama tawala kinachoiunga mkono Urusi, Georgian Dream ambao umekwamisha mchakato wa Georgia kuelekea kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Soma pia: Waandamanaji Georgia wakabiliana na polisi 

Shirika la habari la Associated press limeripoti kuwa waandamanaji hao wanasema chama tawala kimeisaliti Georgia na kuirudisha nchi hiyo kwenye uhusiano wa karibu na Urusi.

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, msemaji wa mkuu mpya wa sera za nje za Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, ametaja ripoti za kutisha za kukamatwa kiholela, vurugu, na unyanyasaji wa waandamanaji na kuhimiza pande zote kutojihusisha na vurugu.

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW