1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano yaendelea mjini Tehran na miji mingine

4 Januari 2026

Maandamano ya hapa na pale yalizuka tena katika mji mkuu wa Iran Jumamosi jioni, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, ambavyo pia vimeripoti mapigano makali kuongezeka magharibi mwa nchi.

Iran Teheran 2025 | Maandamano dhidi ya mgogoro wa kiuchumi na kuporomoka kwa sarafu
Maandamano dhidi ya mgogoro wa kiuchumi na kuporomoka kwa sarafu TehranPicha: Fars News Agency/ZUMA/IMAGO

Maandamano ya hapa na pale yalizuka tena katika mji mkuu wa Iran Jumamosi jioni, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, ambavyo pia vimeripoti mapigano makali kuongezeka magharibi mwa nchi.

Maandamano hayo yalianza Jumapili iliyopita wakati wamiliki wa maduka walipoanzisha mgomo kutokana na wasiwasi wa kiuchumi, lakini tangu wakati huo yameenea kwa ukubwa na malengo huku waandamanaji wakitoa madai ya kisiasa.

Kwa mujibu wa makadirio ya shirika la habari la AFP, maandamano hayo yameathiri kwa viwango tofauti angalau miji 40, hasa ile ya ukubwa wa kati na iliyoko magharibi mwa nchi. Takribani watu 12 wameuawa, wakiwemo wanajeshi wa vikosi vya usalama.

Shirika la habari la Fars, limeyaelezea maandamano ya jana jioni mjini Tehran kuwa "madogo” kwamba yalihusisha makundi ya vijana 50 hadi 200.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW