1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maaskofu wa Katoliki Afrika wapinga kubariki ndoa za mashoga

Sylvia Mwehozi
12 Januari 2024

Maaskofu wa Kikatoliki wa Afrika wamesema kuwa idhini iliyotolewa hivi karibuni na Vatican ya kubariki wapenzi wa jinsia moja haikuwa sahihi kwa bara hilo kwani inakinzana na maadili na utamaduni wa mwafrika.

Maaskofu wa kiafrika
Maaskofu wa Kiafrika wakiingia kanisa kuu la St. Peter Vatican 2009Picha: AP

Maaskofu wa Kikatoliki wa Afrika wamesema kuwa idhini iliyotolewa hivi karibuni na Vatican ya kubariki wapenzi wa jinsia moja haikuwa sahihi kwa bara hilo kwani inakinzana na maadili na utamaduni wa mwafrika.

Kongamano la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar SECAM, limesema katika taarifa yake kuwa mafundisho ya kanisa kuhusu ndoa na kujamiiana bado hayajabadilika.

Maaskofu hao wamesisitiza kwamba hawatobariki ndoa za mashoga kwani kwa kufanya hivyo watazusha taharuki miongoni mwa waumini. Mwezi uliopita kanisa katoliki lilisema kuwa mapadri wanaweza kubariki wapenzi wa jinsia moja chini ya mazingira fulani.

Uamuzi huo wa Vatican umepingwa vikali na nchi za Malawi, Nigeria, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ushoga bado ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi za Kiafrika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW