Maaskofu wajadili hali ya Wakatoliki katika mashariki ya kati
11 Oktoba 2010Wachungaji wakuu kabisa hawasau hata makundi yao madogo ya kondoo, na ndipo siku ya Jumapili tarehe 10 mwezi wa huu, ulianza mjini Vatican mkutano wa maaskofu kuangalia hali ya waumini wa kanisa Katoliki katika eneo la mashariki ya kati. Kiongozi wa kanisa Katoliki Benedict wa 16 anatoa wito kwa dini zote , kuwa na maridhiano pamoja na kuwajibika kisheria.
Mkutano wa majimbo ya kanisa Katoliki kwa ajili ya walio wachache. Kwa ajili ya kuendelea kupungua kwa waumini. Asilimia 1.6 ya watu katika mashariki ya kati ni waumini wa kanisa Katoliki, ambao katika maeneo ya mataifa ya ghuba wanaongezeka waumini hao kutokana na wahamiaji kutoka bara la Asia, lakini wakati huo huo kutoka Iraq waumini wengi wanakimbia. Hata katika nchi ambayo ina waumini wengi Wakikristo kama Lebanon , idadi inazidi kupungua ya Wakatoliki, analalamika mchungaji Tony Cadra.
Tunapaswa kusitisha hali ya Wakristo kutoka katika dini. Pia hakuna mahitaji ya vitabu pamoja na ushauri. Tunahitaji mkakati, ili kuweza kuendelea kuwa na Wakristo katika mashariki ya kati, kwa kuwa hawa ni daraja baina ya dini na mataifa.
Katika makao makuu ya kanisa Katoliki, Vatican hakuna mtu anayechoka kusisitiza , kwamba sinodi hii haina matokeo ya lengo la kisiasa , badala yake ni kwa ajili tu ya malengo ya kiroho. Hata Pope Benedict, amerudia tena siku ya Jumapili katika mahubiri yake wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Ndio sababu anapotoa miito yake mingi ya uhuru zaidi wa kidini pamoja na kuvumiliana katika mashariki ya kati anachukua tahadhari sana. Benedickt anakumbuka wakati akitoa mahubiri kwa lugha zote duniani.
Mkutano huu wa maaskofu wa majimbo ni nafasi katika njia ya kanisa kuweza kufufua imani ya Pentekosti ya siku ya kushuka kwa roho mtakatifu, ili kutangazwa habari nzuri kuwa huru na kuwafikia watu wote.
Siasa za busara pia ni mada nyingine kubwa ya pili katika mkutano huu, siasa ambazo hadi sasa zimeendeleza mzozo wa mashariki ya kati. Hapo kabla mataifa ya Kiarabu yamekuwa na wasi wasi kuwa mkutano huu unaweza kutambua taifa la Israel. Katibu mkuu wa mkutano huo , askofu mkuu wa Croatia Nikola Eterovic, ameepuka mwanzoni mwa mkutano huo kutaja upande wowote pamoja na kutaja jukumu la Wakristo katika mchakato wa amani katika ardhi hiyo takatifu.
Wakristo katika mashariki ya kati ni wanaharakati wa kupigania amani na wanaoleta maridhiano, vitu ambavyo vinahitajika sana katika eneo hilo. Wanamatamanio ya kuishi kwa amani na majirani zao Wayahudi na Waislamu. Kuheshimu sheria hususan sheria za msingi za uhuru wa kidini na moyo safi.
Mkutano huu wa sinodi unahuzunishwa na athari zinazotokana na mzozo kati ya Palestina na Israel na kuathiri maisha ya Wakristo wengi Waarabu. Kukaliwa kwa ardhi ya wapalestina na Israel kunafanya maisha kuwa magumu, kuzuwia uhuru wa kwenda watakako, kuzuwia ukuaji wa uchumi pamoja na shughuli mbali mbali.
Mwandishi : Kleinjung , Tilmann / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri : Mohammed Abdul Rahman