1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAASTRICH: Waandmanaji wapinga ziara ya Bush nchini Uholanzi

8 Mei 2005

Rais George W.Bush wa Marekani amewasili katika mji wa Maastrich kusini mwa Uholanzi.Leo atakutana na Malkia Beatrix wa Uholanzi na waziri mkuu Jan Peter Balkenende.Kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha mwaka wa 60 tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili barani Ulaya,watayazuru makaburi ambako kumezikwa kiasi ya Wamarekani 8,000 waliofariki vitani.Baadae Bush ataelekea Russia na Georgia.Kwa upande mwingine waandamanaji waliohamakishwa na vita vya Iraq vilivyoongozwa na Marekani,walikusanyika mjini Amsterdam kwa mamia kuipingia ziara ya mwanzo kufanywa na Rais Bush nchini Uholanzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW