1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani bado yakabiliana na mafuriko

3 Januari 2024

Utabiri wa hali ya hewa unaashiria kwamba mvua zinazoendelea kunyesha zitaongezeka pamoja na mafuriko. Hali hiyo imesababisha wasiwasi kwa wakazi wa jimbo la kaskazini mwa Ujerumani la Lower Saxony.

Hochwasser in Deutschland
Picha: Gottfried Czepluch/IMAGO

Mashamba katika mikoa kadhaa ya jimbo la kaskazini la Lower Saxony yamefunikwa na maji na kuonekana kama maziwa baada ya mto wa Elbe kufurika.

Vilevile baadhi ya sehemu katika majimbo ya North Rhine -Westfalia, Saxony-Anhalt na Thuringia pia zimeathirika na mafuriko.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, alipotembelea mji wa Verden uliokumbwa na mafuriko katika jimbo la North Rhine -Westfalia, tarehe 31. Desemba 2023.Picha: Fabian Bimmer/REUTERS

Mamlaka ya serikali za mitaa zimesema kima cha maji ya mafuriko bado hakijapungua katika jimbo la Lower Saxony huku miji iliyoathirika zaidi ikiwa ni pamoja na Aller, Leine, Oker na Mittelweser.

Tazama:

Kulingana na idara ya Huduma ya Hali ya Hewa ya Ujerumani (DWD), mvua kubwa inatarajiwa kuendelea kunyesha katika jimbo hilo la Lower Saxony.

DWD imesema baada ya mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha wa kuamkia Jumatano 03.01.2024 iliyoandamana na upepo mkali, hali hiyo imesababisha mafuriko katika baadhi ya sehemu za Lower Saxony na Bremen na itaendelea hadi Alhamisi na huko Thuringia itaendelea hadi Ijumaa.

Soma Pia:Mvua kubwa na mafuriko yasababisha maafa nchini Ujerumani

Wakati wa ziara yake katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko katika jimbo la Lower Saxony, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, aliwashukuru wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada, polisi, idara ya zima moto, watu wanaojitolea na idara ya ufundi. Scholz pia ameahidi msaada wa serikali.

Bavaria, Ujerumani: Huu ni Mto Isar ulio mjini Munich unaonyesha kiwango cha maji kilichopanda.Picha: Sachelle Babbar/ZUMA/IMAGO

Wataalamu nchini Ujerumani wamehimiza juu ya kutathminiwa upya mikakati ya ulinzi wakati wa mafuriko kutokana na hali ilivyo katika baadhi ya maeneo nchini humo ambayo bado yanakabiliwa na hali mbaya ya hewa.

Soma Pia:Wataalamu waonya kitisho cha mafuriko nchini Ujerumani

Mtaalamu katika Kituo cha Helmholtz cha Utafiti wa Mazingira, Ralf Merz, anayefuatilia jinsi mafuriko na mabadiliko ya hali ya hewa yanavyoathiri wingi wa maji.

Amesema kutokana na hali hiyo ambapo michakato ya mafuriko inabadilika, jamii itarajie mafuriko zaidi katika siku za usoni.

Soma Pia:Euro milioni 400 kusaidia wahanga wa mafuriko Ujerumani

Kwa mujibu wa ofisi ya usimaizi wa maji katika jimbo la Lower Saxony, mito mingi bado ina kiwango cha juu cha maji kufikia ngazi ya 3, ambayo ina maana kwamba ipo hatari ya kutokea mafuriko makubwa.

Chanzo:DPA

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW