1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabadiliko ya tabia nchi ni kitisho cha usalama wa chakula

12 Desemba 2023

Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani - WFP mjini Berlin, Martin Frick ametoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa kulinda mazingira.

Usalam wa Chakula | Mkuu wa ofisi ya WFP mjini Berlin,  Martin Frick
Mkuu wa ofisi ya WFP mjini Berlin,  Martin Frick Picha: DW


Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa mazingira wa COP 28 mjini Dubai, Frick amesema bado dunia ina miaka sita hadi saba ya kubadilisha muelekeo wa mabadiliko ya tabia nchi akisisitiza kuwa muda huo ukimalizika kutakuwa na matokeo yasiokuweza kurekebishwa.    


Ameongeza kuwamabadiliko ya tabia nchi ni kitisho kikubwa cha usalama wa chakula. Frick amesema mfumo wa chakula ulioko sasa sio wa uzalishaji, umebakia tu kuwa wa usambazaji na hilo linatishia pia kuwa na upungufu wa chakula. 

Soma pia:WFP: Njaa kali itaongezeka nchini Somalia kufuatia mafuriko

Wawakilishi kutoka mataifa 200 duniani wanahudhuria mkutano huo wa kilele katika mji wa Dubai, unaotarajiwa kumalizika leo  Jumanne.