1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUgiriki

Mabaharia 12 wanatafutwa mkasa wa kuzama meli Ugiriki

27 Novemba 2023

Baharia mmoja amepoteza maisha na wengine 12 hawajulikani waliko baada ya meli moja ya mizigo kuzama kiasi umbali wa kilometa 9 kutoka kisiwa cha Lesbos ambacho ni sehemu ya Ugiriki.

Ugiriki | Ajali ya kuzama kwa meli kisiwani Lesbos
Manusura aliyeokolewa katika mkasa wa kuzama kwa meli ya mizigo kisiwa cha Lesbos akipelekwa hospitali. Picha: Manolis LAGOUTARIS/AFP

Taarifa hizo zimeripotiwa na kituo cha redio cha Ugiriki kikinukuu duru kutoka kikosi cha walinzi wa pwani.

Helikopta ya uokoaji ilifanikiwa kumuokoa mtu mmoja tu ilipokwenda kutoa msaada wa dharura baada ya kupotea taarifa juu ya kuzama kwa meli hiyo iliyokuwa safarini  kutoka Misri kuelekea Uturuki. 

Matumaini ya kuwapata manusura wengine yalikuwa yamefifia usiku wa kuamkia leo kutokana na hali mbaya ya hewa baharini hususani upepo na mawimbi makubwa.

Walinzi wa pwani wamesema meli hiyo iliyokuwa ikipeperusha bendera ya visiwa vya Comoro ilitoa taarifa ya kuwepo hitilafu ya injini na baadaye ilituma ujumbe wa kuhitaji msaada wa dharura kabla ya kupotea kwenye rada.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW