1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabalozi wa NATO kukutana na wenzao wa Ghuba

Josephat Charo
11 Machi 2026

Mabalozi wa jumuiya ya kujihami ya NATO watakutana na wenzao wa nchi za Ghuba kuijadili hali ya vita vinavyoendelea nchini Iran.

Vita vya Iran vimeibua hoja za kujadiliwa na mabalozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami NATO
Vita vya Iran vimeibua hoja za kujadiliwa na mabalozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami NATOPicha: DVIDS/REUTERS

Mabalozi kutoka nchi 32 wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO wanapanga kukutana na wawakilishi wa eneo la Ghuba wiki ijayo kujadili vita vya Iran na mvutano wa kikanda.

Hayo ni kwa mujibu wa wanadiplomasia watatu wa Ulaya walipozungumza na shirika la habari la Reuters.

Wanadiplomasia hao walisema mabalozi hao wanatarajiwa kufanya majadiliano na wenzao kutoka Bahrain, Kuwait, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW