Mabalozi wa nchi za Umoja wa Afrika wamekutana leo mjini Kampala
20 Julai 2010Matangazo
Mabalozi wa nchi za Umoja wa Afrika wamekutana leo mjini Kampala Uganda kuandaa ajenda ya kikao cha mawaziri wa umoja huo kinachotarajiwa kufanyika hapo kesho mjini humo. Mabalozi hao wamebadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ambayo wangependelea yajadiliwe hatimaye na wakuu wa nchi na serikali za Umoja wa Afrika katika mkutano wao uliopangwa kufanyika Jumamosi ijayo mjini Kampala.
Josephat Charo amezungumza na balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, mheshimiwa Mohammed Maundi, na kwanza kumuuliza masuala yaliyoyajadili katika kikao chao cha leo.
Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Abdulrahman