Mabenki 7 ya Ulaya yako hatarini
24 Julai 2010Benki ya serikali ya Hypo Real Estate pekee ya hapa Ujerumani ndiyo iliyoingia kwenye orodha hiyo.Benki hiyo ilitaifishwa mwaka 2008.Taasisi nyengine zilizoingia kwenye orodha hiyo ni benki inayosimamiwa na serikali ya Ugiriki ya ATE na mabenki mengine matano madogo ya Uhispania.Mabenki hayo yameamriwa kuuongeza mtaji wao hadi ufikie kiasi cha dola bilioni 3.5.Lengo la tathmini hiyo lilikuwa kuugundua uwezo wa mabenki wa kuhimili misukosuko ya kiuchumi kadhalika kuwatia imani zaidi wawekezaji katika eneo la mataifa yanayotumia sarafu ya euro.
Hata hivyo bado kuna masuala yaliyojitokeza kuhusu tathmini yenyewe.Shirika la Kimataifa la Fedha ,IMF limeyapongeza matokeo ya tathmini hiyo.Kwa upande wake Waziri wa Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble ameipongeza hatua hiyo na kuielezea kuwa ya kuimarisha imani katika masoko ya fedha.