mabilioni ya yuro kuinusuru dunia isiangamie kwa joto
8 Aprili 2007Matangazo
Berlin:
Kwa mujibu wa ofisi kuu inayoshughulikia usafi wa mazingira
,Ujerumani inabidi kutumia yuro bilioni nne kwa mwaka kuweza
kukabiliana ipasavyo na mabadiliko ya hali ya hewa.Mataifa ya viwanda
yanabidi yapunguze kwa asili mia 80 moshi unaotoka viwandani hadi
ifikapo mwaka 2050- amesema mwenyekiti wa taasisi hiyo bwana
Andreas TROGE katika mahojiano na gazeti la “BILD am
SONNTAG.”Kitisho cha kuzidi hali ya ujoto duniani kinaweza tuu
kuzuwilika kwa kutolewa vitega uchumi kwa wingi-amesema.Fedha hizo
zitabidi zitumiwe katika nishati mbadala-anahimiza bwana Troge.Waziri
wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani anatetea umuhimu wa
kuendelea kutumiwa kinu cha nishati ya kinuklea nchini Ujerumani.