1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabingwa watetezi Marekani walenga kufuzu duru ya mtoano

31 Julai 2023

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia kwa wanawake, Marekani, hapo Jumanne watakuwa wanaingia uwanjani kucheza mechi yao ya mwisho ya makundi watakapokwaana na Ureno.

Neuseeland Fussball Frauen WM 2023 l USA vs Niederlande l Alex Morgan
Picha: Ira L. Black/Zuma Wire/IMAGO

Kocha wa kina dada wa Marekani Vlatko Andonovski amesema kwamba mechi hiyo haitokuwa rahisi licha ya kuwa timu yake ndiyo inayopigiwa upatu kupata ushindi.

"Kwetu sisi cha muhimu bila shaka ni kufika awamu ya mtoano kwanza na hicho ndicho kilicho akilini kwa sasa. Hatutaki kuangalia mengine. Hatutaki kutazama hatua mbili, tatu au nne mbele, hii ndiyo hatua ya kwanza. Wacha tuhakikishe kwamba tumefuzu, kwasababu tukianza kufikiria mbele zaidi, huenda tusifanikiwe," alisema Andonovski.

Marekani watahitajika kupata pointi tatu katika mechi ya keshi na kupata magoli mengi ili washinde kundi lao G.

Vyanzo: Reuters/DPAE/AP

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW