1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoMarekani

Marekani watupwa nje Kombe la Dunia na Sweden

7 Agosti 2023

Licha ya kuwa nambari moja kwenye viwango vya ubora duniani vya FIFA, mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia la Wanawake Marekani wametupwa nje ya mashindano hayo katika hatua ya 16 bora na Sweden.

Australien FIFA Frauen-Weltmeisterschaft 2023 Schweden gegen den USA im Melbourne
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Marekani Megan Rapinoe akisononeka baada ya kukosa penati kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.Picha: James Ross/AAP/IMAGO

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia la Wanawake Marekani wametupwa nje ya michuano hiyo.

Michuano ya Kombe la Duniani kwa Wanawake bado inaendelea nchini Australia na New Zealand na ulimwengu unaendelea kushuhudia matokeo ya kushangaza mara baada ya mabingwa watetezi Marekani kutolewa nje ya mashindano hayo katika hatua ya 16 bora na Sweden kupitia mikwaju ya penalti huko mjini Melbourne.

Soma zaidi:Nigeria yaaga Kombe la Dunia la Wanawake

Marekani walitawala karibu dakika zote 120 za mchezo huo lakini mechi iliishia kumalizika bila bao na kupelekea penalti kuamua matokeo ambapo Sweden walifunga penalti 5 dhidi ya 4 za Marekani.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Wanawake ya Sweden wakifurahia kufuzu hatua ya robo fainali kwa kuwatoa Marekani ambao ni mabingwa watetezi.Picha: Joel Carrett/AAP/IMAGO

Nyota wa Marekani Megan Rapinoe aliyekuwa anacheza kombe lake la mwishio alikosa penati, pamoja na wachezaji wengine watatu wa Marekani na kuipa nafasi Sweden ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Soma zaidi:Kenya: Waathirika wa mashambulizi ya ubalozi wa Marekani bado kufidiwa 

Marekani inayoongoza kwa viwango vya ubora duniani vya FIFA kwa upande wa wanawake inaungana na mataifa mengine makubwa kama Ujerumani na Italia ambayo yametupwa nje ya mashindano hayo.

Sweden sasa itacheza robo fainali na Japan ambayo imeitoa Norway siku ya Ijumaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW