1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNICEF: Waasi wawavisha watoto mabomu nchini DRC

8 Septemba 2023

Umoja wa Mataifa umesema leo kwamba waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliwafunga pacha vichanga wa kike mikanda yenye vilipuzi kama mtego kwa vikosi vya usalama.

DR Kongo Soldaten
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Mwakilishi wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF nchini Congo, Grant Leaity, amewaambia waandishi wa habari kwamba lengo lilikuwa kwamba punde polisi au wanajeshi wa Congo wangefika karibu na watoto hao, wangelipua mabomu hayo.

Kisa hicho ni kati ya matukio yayoonyesha  ongezeko la ukatili dhidi ya watoto  nchini humo. Wasichana hao wenye umri wa mwaka mmoja walipatikana katika kijiji kilichoko kaskazini mwa Kivu.

Shirika la UNICEF, limesema wanamgambo wa ADF wamekuwa wakiongeza mashambulizi ya mabomu katika eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW