MACHAFUKO KISIWANI HAITI:
8 Januari 2004Matangazo
PORT AU PRINCE: Watu 2 wameuawa katika mji mkuu wa Haiti-Port au Prince baada ya risasi kufyetuliwa wakati wa maandamano.Watu wengine 13 pia wamejeruhiwa katika wimbi jipya la maandamano ya kuipinga serikali ya Rais Jean Betrand Aristide.Upande wa upinzani umemtuhumu Aristide kwa makosa ya ulaji rushwa na maongozi maovu na umetoa muito kuwa aondoke madarakani.Lakini Aristide ambae bado ana miaka miwili ya kipindi chake cha miaka mitano madarakani,amekataa kuondoka.