1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko mapya yaripotiwa Syria

28 Desemba 2025

Ghasia zimezuka nchini Syria kati ya wafuasi na wapinzani wa serikali ya Syria, na kusababisha majeruhi kadhaa katika mfululizo wa machafuko unaoendelea tangu kuondolewa madarakani kwa Bashar al‑Assad mwaka jana.

Syria  Homs 2025 |
Serikali, imedai kuwa wafuasi wa al‑Assad waliwashambulia maafisa wa usalama na kuharibu magari ya polisi.Picha: Omar Haj Kadour/AFP

Kundi la ufuatiliaji la Syrian Observatory for Human Rights limesema waandamanaji angalau wanane wa kupinga serikali walijeruhiwa katika eneo la Latakia baada ya kushambuliwa na wafuasi wa serikali na vikosi vya usalama.

Maandamano hayo yalienea hadi miji ya Tartus, Homs na Hama, yakichochewa na wito wa kiongozi wa jamii ya Waalawi, Ghazal Ghazal, kudai haki ya kujitawala.

Serikali, kupitia mkuu wa usalama wa Latakia, Brigedia Abdel‑Aziz al‑Ahmad, imedai kuwa wafuasi wa al‑Assad waliwashambulia maafisa wa usalama na kuharibu magari ya polisi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW