Machafuko mjini Kampala, nchini Uganda
11 Septemba 2009Matangazo
Habari zilisema kiasi ya watu saba waliuawa katika ghasia hizo zinazotokana na hasira za wafuasi wa Mfalme Ronald Mutebi wa wabaganda baada ya serikali kumzuwia kulizuru eneo la Kayunga kaskazini mwa Kampala na kusababisha mvutano kati ya Wabaganda na Wabanyala.Nilizungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mkaazi wa Kampala Badrudin Khalfan ambaye kwanza alinielezea chanzo hasa cha mfutano kati ya Wabaganda na Wabanyala na kama kuna mkono wowote wa kisiasa.