1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yaendelea kushuhudiwa Msumbiji

Hawa Bihoga
3 Novemba 2024

Polisi nchini Msumbiji imetumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji katika miji kadhaa, wanaopinga matokeo ya uchaguzi wenye utata.

Msumbiji I Waandamanaji wakiwa mitaani
Muandamaji akiwa anapeperusha bendera ya msumbijiPicha: Alfredo Zuniga/AFP

Machafuko yamelikumba taifa hilo la Kusini mwa Afrika tangu kumalizika kwa uchaguzi mnamo Oktoba 09 ambao ulikipa ushindi chama tawala cha Frelimo kilichokuwa madarakati tangu mwaka 1975 lakini ukilaaniwa na vyama vya upinzani vinavyodai kuwepo na udanganyifu.

Soma pia:Chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji chaomba kura kuhesabiwa upya

Asasi moja ya kiraia imeliambia shirika la habari la AFP kwamba katika mkoa wa Nampula ambao ni kitovu cha machafuko polisi ilitumia nguvu kuwatawanya waandamaji ikiwemo mabomu ya kutoa machozi.

Polisi haijazungumza chochote kuhusu shutuma za kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW