1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yaendelea kwa usiku wa tatu nchini Ufaransa

28 Novemba 2007

Vijana katika vitongoji vya mji mkuu Paris nchini Ufaransa wameendelea kufanya machafuko kwa usiku wa tatu mfululizo. Machafuko yameenea kufikia mji wa kusini wa Toulouse.

Hata hivyo idadi kubwa ya maafisa wa polisi waliotumwa kushika doria katika vitongoji hivyo, imesaidia kupunguza machafuko ya usiku wa leo yakilinganishwa na machafuko ya siku mbili zilizopita yaliyofanywa katika kitongoji cha Villiers-le-Bel.

Katika mji wa kusini wa Toulouse, polisi wanasema motokaa 10 zimechomwa moto pamoja na maktaba moja.

Rais wa Ufaransa, Nicholas Sarkozy, ametoa mwito kuwe na utulivu na anatarajiwa kufanya mkutano wa dharura na serikali yake.

Machafuko ya sasa yalianza baada ya vijana wawili kufariki wakati pikipiki yao ilipogogana na motokaa ya polisi.