1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yafuatia kuthibishwa kwa kifo cha John Garang

Gregoire Nijimbere1 Agosti 2005

Kifo cha John Garang kimepokelewa kwa uzuni mkubwa hususan mjini Khartoum ambako wafuasi wake wamezusha machafuko.

Garang bega kwa bega ba rais El Bashir
Garang bega kwa bega ba rais El BashirPicha: AP

Mara tu baada ya kifo chake kuthibitishwa rasmi, maelfu ya washabiki wake wametelemka bararani katika mji mkuu Khartoum kwa maandamano ambayo yamekumbwa na machafuko. Wakiwa na visu na vyuma, wafuasi wa John Garang, wamewapiga watu, kuyavunja maduka na magari na hata kuzichoma moto.

Mkaazi mmoja wa mjini Khartoum amesema kuwa ameziona maiti za watu wawili ambao waliuawa. Shahidi mungine ambae ni mwanafunzi amesema na hapa ninamnukuu “Watu walikuwa wakikimbia katika barabara zote, wakimpiga yeyote yule anayefanana na muarabu”.

Upande wa kusini hali ni tulivu kiasi katika mji wa Rumbek ambako maiti ya Garang imefikishwa leo. Maelfu ya wafuasi wa SPLM, wamekusanyika kwa uzuni mkubwa mjini humo uwanja wa uhuru. Mji wa Rumbek ulukiwa makao makuu ya Garang na makao makuu ya muda ya serikali ya kijimbo ambayo ingaliundwa kabla ya kuhamia katika mji mkubwa wa eneo la kusini wa Juba, ambako kumearifiwa vurugu pia.

Kasisi wa kianglikana Paul Yugusuk, amesema kuwa amepata taarifa za ghasia mjini Juba. Pia milio mingi ya risasi imeskika katika mji huo, lakini taarifa zinasema risasi zilikuwa zikifiatuliwa hewani kama heshima kwa marehemu kiongozi wao.

Viongozi kadhaa nchini Sudan na nje ya Sudan wameelezea maskitiko yao. Rais Omar El Bashir ambae alisaini wiki tatu tu zilizopita katiba mpya na John Garang, amesema anayo imani kubwa kuwa mpango wa amani utaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake naibu wa John Garang ambae anaweza kuwa mrithi kukiongoza chama cha SPLM, Salva Kiir Mayardit, ametuliza nyoyo kwamba viongozi na maafisa katika chama, watadumisha umoja na kuendeleza sera za kiongozi wao.

Waziri wa Uganda wa mambo ya kigeni Sam Kutesa ameitaja ajali hiyo ambamo John Garang ameuliwa kuwa ni tukio baya, msiba mkubwa ambao umeikumba siyo tu Sudan bali pia kanda nzima.

Rais wa Kenya Mwai Kibaki amesema kuwa ameskitishwa na kifo cha John Garang na kuwasihi raia wa Sudan wasivunjiki moyo katika juhudi zao za kusaka amani.

Thabo Mbeki rais wa Afrika ya kusini, amesema kuwa kifo cha Garang ni pigo kubwa lakini kwamba itabidi nia yake iendelezwe. Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi za kiarabu, wanasema Garang alikuwa na jukumu muhimu katika mpango wa amani ya Sudan. Sasa na la muhimu ni kuwaunga mkono raia wa Sudan wazidi kusonga mbele.

Wataalamu wa masuala ya kisiasa, wanaona kuwa Garang angelichangia pia katika kuusuluhisha mzozo wa magharibi katika jimbo la Darfur.

Wanaona pia kuna hatari kukazuka uhasama wa urithi ndani ya chama cha SPLM, japokuwa viongozi wote wamehakikisha kudumisha umoja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW