1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko yaibuka Msumbiji, ikisubiri matokeo ya uchaguzi

14 Oktoba 2023

Chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji kimedai kupata ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa jana Ijumaa katika maeneo kadhaa ukiwemo mji mkuu Maputo na kuibua ghasia katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Mosambik Maputo | Wahlen | Anhänger des nationalen mosambikanischen Widerstands
Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji, RenamoPicha: Alfredo Zuniga/AFP

Matokeo ya awali yaliyotolewa jana Ijumaa yalionyesha kuwa chama cha upinzani Renamo kimepata zaidi ya asilimia 52 ya kura mjini Maputo, huku Frelimo ikipata chini ya asilimia 40, na hivyo kuupa upinzani ushindi ambao haujawahi kushuhudiwa.

Soma pia: Rais wa Msumbiji awatimua mawaziri sita serikalini

Chama cha upinzani cha Renamo hakijawahi kushinda uchaguzi wa katika nchi hiyo iliyopata uhuru mwaka 1975 kutoka kwa Ureno. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa siku chache zijazo, huku tume ya uchaguzi ikisisitiza kwenye mitandao ya kijamii kwamba raia watapaswa "kuheshimu matokeo".

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW