1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Machafuko yaibuka tena katika mji mkuu wa Sudan

16 Julai 2023

Mashambulizi ya anga yamerindima leo katika mji mkuu wa Sudan Khartoum, huku mapambano yakishika kasi magharibi mwa Darfur.

Sudan | Kämpfe in Khartoum
Picha: - /AFP/Getty Images

Mashuhuda wameliambia shirika la habari la AFP kuwa ndege za kivita za jeshi zilizilenga kambi za kikosi cha wanajeshi wa dharura cha RSF, mashariki na kusini magharibi mwa Khartoum ambapo kikosi hicho kilijibu mashambulizi.

Soma pia: ICC yaanzisha uchunguzi mpya katika machafuko ya Sudan

Taarifa zaidi zinasema droni za  RSF zilielekeza mashambulizi katika hospitali kubwa ya jeshi mjini Khartoum. Shambulio la aina hiyo lilifanywa Jumamosi katika hospitali hiyo hiyo tukio lililosababisha vifo vya watu watano na kuwajeruhi wengine 22.

Takwimu za Umoja wa taifa zinaonesha kuwa, Hadi sasa vita kati ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na aliyekuwa msaidizi wake anayekiongoza kikosi cha RSF Mohammed Hamdan Daglo vimeshasababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 na kusababisha wengine milioni 2.5 wayakimbie makazi yao.