SiasaEcuador
Machafuko yasababisha vifo vya wafungwa 31 gerezani Ecuador
10 Novemba 2025
Matangazo
Wafungwa 31 mmoja wamefariki katika gereza moja nchini Ecuador.
Hayo yamesemwa na mamlaka ya gereza SNAI, na kueleza kuwa, wafungwa 27 waliokufa waligunduliwa Jumapili jioni.
Kulingana na maafisa hao, wafungwa hao walikufa kwa kukosa hewa kwa sababu ya kujinyonga au kunyongwa. Lakini haijabainika kikamilifu matukio yaliyosababisha vifo vyao.
Awali, mamlaka hiyo iliripoti kwamba wafungwa wanne waliuawa wakati wa machafuko ndani ya gereza hilo lililoko mji wa pwani ya Ecuador, Machala. Mamlaka hiyo imesema Idara husika zimeshaanza uchunguzi kuhusu kisa hicho.
Watu wengine 34 walijeruhiwa akiwemo afisa wa polisi wakati wa machafuko hayo.