Machafuko yazuka Senegal
28 Januari 2012Waandamanaji waliwarushia mawe polisi ambao walijibu kwa kufyatua mabomu ya machozi huku kukiwa na ripoti ya kifo cha polisi mmoja.
Shirika la habari la Reuters limesema, maripota wake wamewashuhudia vijana wakichoma moto matairi na kupindua magari, baada ya uamuzi huo kutolewa jana jioni. Wapinzani wa Wade mwenye umri wa miaka 85 wamesema, katiba hairuhusu kushika wadhfa wa urais kwa zaidi wa mihula miwili. Wade alieshika madaraka 2000 na kuchaguliwa tena 2007, amesema, awamu yake ya kwanza ilikuwa kabla ya mageuzi ya katiba ya mwaka 2001 yaliyoweka kiwango hicho.
Mahakama Kuu imewaidhinisha wagombea wengine 13 lakini wamepinga ombi la muimbaji maarufu Youssou N´Dour anaetaka kugombea urais. Kwa mujibu wa mahakama muimbaji huyo hajakusanya saini 10,000 zililizothibitisha kumuunga mkono, kama inavyohitajiwa.