Machar yuko tayari kujibu kesi inayomkabili
20 Septemba 2025
Matangazo
Kur Lual Kur amesema mshtakiwa yuko tayari kwa kesi na pia kwamba yuko katika afya njema.
Alithibitisha kuwa Machar atahudhuria kikao hicho cha kwanza maalum cha mahakama siku ya Jumatatu kufuatia wito uliotolewa lakini akasema bado wanasubiri maelezo zaidi.
Upande wa utetezi umekanusha mashtaka dhidi yake yanayojumuisha mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu pamoja na madai kwamba aliagiza wapiganaji wa kikabila kushambulia kambi moja ya kijeshi mwaka huu na kusema ni sehemu ya juhudi za Rais Salva Kiir za kuutenga upinzani na kudumisha mamlaka.