Macron aanza ziara ya siku tano katika Bahari ya Hindi
21 Aprili 2025
Matangazo
Macron, akiambatana na mkewe Brigitte, atatumia siku moja kukutana na wakaazi na wabunge wa visiwa vya Mayotte na kuchukua tathmini ya ujenzi mpya wa visiwa hivyo, ambavyo bado vinakabiliwa na madhara ya Kimbunga Chido kilichopiga eneo hilo mnamo Desemba mwaka jana.
Rais Macron anawasili na rasimu ya sheria ya "kujenga upya" visiwa hivyo, ambayo inalenga pia kuimarisha vita dhidi ya uhamiaji haramu, makazi haramu, ukosefu wa usalama na kufufua uchumi wa ndani.
Baada ya visiwa vya Mayotte na Reunion, Macron atasafiri kwenda Madagascar na Mauritius kushughulikia mada za usalama wa baharini na ulinzi wa bahari, katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa plastiki.