1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron afanya mazungumzo na Rais Xi Jinping mjini Paris

6 Mei 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana hii leo na Rais wa China Xi Jinping kwa mazungumzo mjini Paris, wakati kiongozi huyo wa China akianza ziara rasmi ya kikazi nchini Ufaransa.

Ufaransa | Xi Jinping mjini Paris
Rais wa Ufaranya Emmanuel Macron akisalimiana na mgeni wake, Rais Xi Jinping wa China katika ikulu ya Elysee mjini Paris.Picha: Gonzalo Fuentes/REUTERS

Macron alisalimiana na Xi katika kasri la Elysee, kabla ya kuanza mazungumzo yatakayogubikwa na vita vya Ukraine na mizozo ya kibiashara.

Duru ya kwanza ya mazungumzo itajumuisha pande tatu na kumshirikisha Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen.

Macron amemweleza Xi kwamba ushirikiano na Beijing katika migogoro mikubwa ikiwemo Ukraine ni muhimu na kuhimiza kanuni sawa kwa wote katika uhusiano wa kibiashara baina ya China na Umoja wa Ulaya.

Rais Xi amesema mwanzoni mwa mazungumzo yake mjini Paris kwamba China inaichukulia Ulaya kama kipaumbele chake cha sera ya kigeni na kuutizama uhusiano kati ya pande hizo mbili kuwa wa kimkakati na endelevu.

Xi ameongeza kuwa China na Umoja wa Ulaya zinapaswa kuendelea kujitolea katika ushirikiano wa pande zote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW