1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron aihimiza Ulaya kuharakisha msaada kwa Ukraine

31 Januari 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amewahimiza viongozi wa Ulaya kufanya maamuzi ya kijasiri na ya kibunifu katika miezi michache ijayo ili kuharakisha na kuongeza msaada wao kwa Ukraine.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akilihutubia bunge la Ujerumani
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akilihutubia bunge la Ujerumani Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Akizungumza katika ziara yake ya Sweden, Macron amesema gharama za ushindi wa Urusi ni kubwa mno kwa kila mmoja.

Rais huyo wa Ufaransa ameonya kuwa hakuna mkakati zaidi wa usalama na muundo katika bara la Ulaya ambao utatumika kama Urusi itashinda vita.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakusanyika mjini Brussels leo kwa mkutano na Baraza la Ulaya, ambapo watajadili msaada kwa Ukraine wakati vita hivyo vikikaribia mwaka wake wa pili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW