1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron aisihi China kushinikiza amani Ukraine na kuweka usaw

4 Desemba 2025

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amemsihi Rais wa China, Xi Jinping, kusaidia kumaliza vita vya Ukraine na kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kimataifa, biashara na mazingira.

Beijing, China 2025 | Xi Jinping akimkaribisha Emmanuel  Macron
Ufaransa na China zinapaswa kuonesha ushirikiano unaozingatia sheria za kimataifaPicha: Jeanne Accorsini/SIPA/picture alliance

Akizungumza Alhamisi katika mkutano wao mjini Beijing, Macron alisema anatarajia China iunge mkono juhudi za kufikia makubaliano ya haraka ya kusitisha mashambulizi yanayolenga miundombinu ya kiraia.

"Hili ni muhimu kwa majira yanayokuja ya baridi, kwa kuzingatia kwamba miundombinu ya kiraia, hasa nishati bado inashambuliwa na Urusi. Lakini kwa upana zaidi, tuna matumaini ya kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kupatikana amani ya haki na kudumu, ambayo inaheshimu sheria za kimataifa," alifafanua Macron.

Kwa upande wake, Xi alisema kwamba yeye na Macron wamekubaliana kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, kuongeza uwekezaji wa pande mbili na kuhakikisha mazingira yasiyo ya kibaguzi kwa biashara katika nchi zote mbili.

Pia alisisitiza umuhimu wa kusitishwa kwa uhasama nchini Ukraine, akisema China inaunga mkono juhudi zote za kupatikana kwa amani na ina matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano ya kudumu yanayokubalika na pande husika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW