1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Macron aitetea sheria ya pensheni, maandamano yapangwa

18 Aprili 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameyatetea mageuzi ya mfumo wa pensheni na amesisitiza kwamba kupandisha umri wa kustaafu nchini Ufaransa ni hatua ya lazima.

Frankreich, Paris | Präsident Macron TV-Ansprache zur Rentenreform
Picha: Sarah Meyssonnier/REUTERS

Rais Macron  amesema hayo katika hotuba aliyotoa kwa njia ya televisheni. Ameeleza kwamba ni lazima kupandisha umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64 ili kuepusha kusambaratika kwa mfuko wa malipo ya uzeeni.

Soma pia: Macron asaini sheria tata ya pensheni, maandamano ya ghasia yazuka

Hata hivyo rais huyo amekiri kuwa mageuzi hayo hayaungwi mkono na amesema anatambua kwamba wananchi wamekasirika. Wanaoyapinga mabadiliko hayo nchini Ufaransa wamesema hotuba ya rais Macron haikusaidia kupunguza mivutano na jumuiya za wafanyakazi zimeazimia kuendelea na maandamano ya kupinga mabaidliko hayo.

Wakati rais Macron akitoa hotuba waandamanaji waliendelea na harakati zao nchini Ufaransa kote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW