Macron alenga kuanzisha upya mahusiano na Rwanda
26 Mei 2021Matangazo
Macron ndiye kiongozi wa kwanza tangu 2010 kuitembelea nchi hiyo ya Afrika, ambayo kwa muda mrefu imeituhumu Ufaransa kwa uzembe katika mauaji ya halaiki ya Watutsi nchini Rwanda yaliotokea mwaka 1994.
Akiwa ziarani nchini Ufaransa wiki iliyopita, Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye kwa wakati mmoja alivunja mahusiano na Ufaransa, alisema nchi hizo mbili zina fursa ya kuwa na uhusiano mzuri.
soma zaidi: Rwanda yailaumu Ufaransa kushindwa kuzuia mauaji ya Kimbari
Kabla ya ziara ya Macron mjini Kigali, nchi hizo mbili zimezungumza kwa shauku nia ya kurejesha mahusiano.
Maafisa wa Ufaransa wanasema Macron huenda pia akaitumia ziara hiyo kumtangaza balozi nchini Rwanda, akijaza nafasi hiyo iliyowachwa wazi tangu 2015.