1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya nyuklia matatani

7 Julai 2019

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amemuonya mwenzake wa Iran Hassan Rouhani, kwamba ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuendelea kudhoofishwa zaidi mkataba wa nyuklia wa Iran uliofikiwa mwaka 2015 na kuonya kuwa madhara yatafuata

Frankreich, Paris: Emmanuel Macron im Elysee Palast
Picha: Getty Images/AFP/L. Marin

Macron, ambae alizungumza na rais wa Iran Rouhani, siku moja kabla ya Iran kujiandaa kuongeza urutubishaji wa madini ya urani kupita kiwango kilichowekwa katika makubalino yake na mataifa makubwa, amesema anataka kuweka msukumo wa kufanyika mazungumzo kuanzia sasa na Julai 15, kwa lengo la kuzirudisha pande zote katika meza za mazungumzo.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa Ufaransa Macron amesema " rais ameonesha wasiwasi mkubwa, kutokana na hatari viashiria vya udhoofishiji wa mkataba wa nyukilia wa mwaka 2015, madhara ambayo yatakufuata" Lakini haijawa wazi kwamba madhara gani hasa ambayo taarifa hiyo inayazungumzia. Hata hivyo maafisa katika ofisi ya Macron, hawakuweza kupatikana kutoa ufafanuzi wa hoja hiyo.

Rais Hassan Rouhani wa IranPicha: Tasnim

Mkwamo wa utekelezaji wa mkataba

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema kuendelea kukiukwa zaidi kwa mkataba huo, kunaweza kusababisha upande wa Ulaya yaani Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kukawepo kwa mtibuano wa muundo wa maazimio ndani ya mkataba wenyewe, jambo ambalo linaweza kuchangia kuzushwa kwa uwekwaji wa vikazo vya Umoja wa Mataifa.

Tangazo la Iran linatolewa katika kipindi ambacho kumekuwa na makabiliano kati ya Iran na Marekani, ikiwa sio kipindi kinachopindukia mwaka tangu serikali ya Marekani ijiondoe katika makubaliano ya nyuklia na kuweka vikwazo ambavyo viliondolewa kwa mujibu wa mkataba wa nyuklia, kwa makubaliano ya Iran kupunguza matumizi yake ya nyuklia.

Masharti ya Iran kwa Ulaya

Iran imetoa takwa la kuitaka mataifa ya Ulaya kufanya jitihada zaidi, katika kuhakikisha Iran inapata manufaa ya kiuchumi, na hasa katika sekta yake ya mafuta ambayo Marekani imekuwa ikiilenga. Macron amsema pamoja na Iran kutoa tarehe ya mwisho ya Julai 7, alkini amekubaliana na Rouhani kufanyika jitihada kuanzia sasa hadi Julai 15, kurejesha mazungumzo kwa pande zote.

Hata hivyo kwa upande wa Iran, haujaonekana kuunga mkono mazungumzo hayo kama vikwazo vyote ilivyowekewa havijaondolewa. Katika  televisheni ya umma ya Iran Rais Rouhani amesikika akisema kuondolewa kwa vikwazo kwa taifa lake kutatoa fursa wa mwelekeo mpya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW