1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron akataa kuunda serikali ya mrengo wa kushoto

27 Agosti 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameondoa uwezekano wa kuteua waziri mkuu mpya kutoka mrengo wa kushoto ili kumaliza mkwamo wa kisiasa, akisema kwa kufanya hivyo kungetishia "utulivu wa taasisi" nchini humo.

EMMANUEL MACRON - DISCOURS APRES LEGISLATIVES ET JO
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Vincent Voegtlin/dpa/MAXPPP/dpa/MAXPPP/picture alliance

Macron amekuwa akifanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wakati akikabiliwa na shinikizo la kuteua waziri mkuu baada ya muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto kupata viti vingi katika duru ya pili ya uchaguzi wa bunge uliofanyika mwezi Julai.

Rais huyo amekataa wazo la mrengo wa kushoto la kuunda serikali baada ya kufanya mazungumzo na mwanasiasa wa mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen na viongozi wengine.

Wakati baadhi ya ripoti zikidai kuwa Macron alitaka kumteua Waziri mkuu leo Jumanne, kiongozi huyo badala yake amesema atafanya duru nyingine ya mazungumzo.

Soma pia: Macron afanya mazungumzo na Le Pen kuhusu Waziri Mkuu

Tangu siku ya Ijumaa, Macron amewaalika viongozi wa kisiasa kwa mazungumzo yenye lengo la kupata mgombea anayeungwa mkono na pande zote.

Uchaguzi wa Julai uliliacha bunge la Ufaransa lenye viti 577 likigawika kati ya muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto wa New Popular Front uliopata zaidi ya viti 190, ukifuatiwa na muungano wa Macron wa mrengo wa kati ukipata takriban viti 160 huku chama cha mrengo mkali wa kulia cha National Rally kikipata viti 140.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW