1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron aonya dhidi ya kuenea siasa za misimamo mikali Ulaya

28 Mei 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametoa wito wa umoja wa Ulaya wakati wa hotuba yake katika mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Dresden.

Rais Macron akihutubia mjini Dresden
Macron yuko katika ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Ujerumani Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Macron amesema utawala wa kimabavu unaweka kitisho kikubwa kwa mustakabali wa Ulaya, akitolea mfano wa kuongezeka kwa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia.

Huku akitaja vita vinavyoendelea nchini Ukraine, Macron amesema Ulaya iko katika njia panda. Amesema kuwa amani, ustawi na demokrasia viko chini ya kitisho kama viongozi hawatachukua hatua.

Soma pia: Macron aupongeza ushirikiano wa Ufaransa na Ujerumani

Macron alitoa hotuba yake katika kanisa maarufu la Frauenkirche mjini Dresden. Kanisa hilo linaashiria uharibifu uliofanywa wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na baadae kuunganishwa tena kwa Ujerumani baada ya kumalizika Vita Baridi. Macron awali aliyatembelea makumbusho ya mauaji ya halaiki ya Wayahudi, Holocaust, mjini Berlin, ambako alitoa heshima zake kwa Wayahudi milioni 6 waliouawa na Manazi.

Hii leo Macron anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya kiserikali ya siku tatu, kwa kuelekea magharibi mwa Ujerumani kukitembelea chuo kikuu cha Münster anakotarajiwa kutunukiwa tuzo ya amani ya kimataifa ya Westphalia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW