1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron apata nguvu za kisiasa

23 Februari 2017

Kampeni ya mgombea wa kiti cha urais wa nchini Ufaransa Emmanuel Macron imepata nguvu mpya baada ya kuungwa mkono na wanasisaia wa mrengo wa wastani.

Frankreich Paris Präsidentschaftskandidat Emmanuel Macron
Picha: Reuters/P. Wojazer

Hali hii inabadilisha sura ya kempeni wakati ambapo mpinzani wake, kiongozi wa  siasa kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen akishitakiwa kwa kashfa ya ajira bandia. 

Ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya Ufaransa kwenda katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkali usiotabirika, mwanasiasa mkongwe wa siasa za wastan Francois Bayrou anatangaza kuungana na Emmanuel Macron katika kile alichokiita kitisho kikubwa cha upande wa wanaofuata mrengo mkali wa kulia. Bayrou aliyezizima kwa miezi kadhaa katika kinyang'anyiro cha urais amehitimisha safari yake kwa kusema hawezi kuendelea kugawanya kura za wenye siasa za wastani jambo ambalo amesema lingemnufaisha Le Pen.

Tangazo lake hilo amelitoa wakati waziri wa zamani wa uchumi Macron, ambae imeshuhudia uungwaji mkono wake ukiongezeka katika wiki za hivi karibuni baada ya mpizani wake mhafidhini Francois Fillon kuchagizwa na tuhuma za  rushwa lakini pia kumjongelea tena nyuma yake katika uchuguzi wa hivi karibuni.

Pigo kwa mgombea Le Pen

Picha: picture alliance/dpa/AA/R. A. Safadi

Mgombea wa chama cha National Front cha siasa kali za kizalendo, Marine Le Pen, vilevile alipata pigo kubwa hapo jana baada ya msaidizi wake Catherine Griest kushitakiwa kwa kukiuka maadili kuhusiana na  tuhuma kwamba Bi Le Pen alifanya udanganyifu katika matumizi ya kiasi cha  euro 340,00 katika bunge la Ulaya. Bunge linamtuhumu Le Pen kwa kutimia fedha hizo kumlipa Griest pamoja na mlinzi Thierry Legier, wakati wakifanya kazi zaidi katika chama chake nchini Ufaransa kuliko ilivyotarajiwa katika bunge la ulaya. .

Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen amejiongezea uongozi wake katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa, ingawa kulingana na uchunguzi wa kura za maoni anaonekana kama atazidiwa nguvu kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi wa marudio. Kiongozi huyo  wa chama cha National Front anaonekana atashinda kwa asilimia 27.5 za kura kwa Aprili, na ikiwa tofauti ya asilimia 2.5 ikilinganishwa na uchaguzi wa Februari 4.

Mwanasisa wa siasa za wastani Emmanuel Macro, kwa mujibu wa uchunguzi huo, anaonekana kujongelea nafasi ya pili kwa asilimia 21 ya kura, nyuma kwa asilimia moja, akifuatiwa na muhamifidhina Francois Fillon mwenye asilimia 19 za kura, ambae pia yuko nyuma kwa nukta moja ya asilimia za kura. Katika uchaguzi wa marudio wa mwezi Mei, Macron anaonekana mwenye kumshinda Le Pen akiwa na asilimia 61 kwa 39.

Hata hivyo uchunguzi huo uliokusanywa Jumapili na Jumatatu, unaonesha hautaathiri chochote katika maendeleo ya kampeni za sasa ambapo imeshuhudiwa Fillon akipanda na kushuka kutokana na kuchunguzwa kwake ya tuhuma ya matumizi mabaya ya fedha kwa kuilipa familia yake.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR/AFP
Mhariri: Gakuba Daniel

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW